Monday, March 4, 2013

MATAPELI SUGU

2013
utapeli upo wa kuchukua pesa
zako cash na utapeli wa
kuchukua vitu/bidhaaa
unazouza,
hawa wajamaa wamebobea
kwenye utapel wa aina zote na
wanatumia uchawi, usipokuwa
makini au kama huna taarifa hao
ni matapeli unalizwa,
nasikia hawa matapeli wa
mtongani walishatolewa hadi
kwenye tv na RPC lakini si wote
waliobahatika kuona hiyo
taarifa na hawa na mtandao
wao wanaendelea kuwaliza
watu, juzi jumatatu tumelizwa
milioni 2 na hawa mbwa,
inauma sana,
kama wewe ni mfanyabiashara,
jihadhari nao watakupigia simu
na kusema wana vitu/vifaa vya
bei rahis wanauza kisha
watakutapeli bila huruma
milions/laki zako ulizotolea jasho
lako,
ukiwa unauza vifaa/vitu
watakupigia simu na kusema
kuna mzee/kaka/baba yao
anataka na kisha kusepa navyo
na kubaki unashangaa
watakupigia simu watakuambia
ushuke mtonngani, ukishuka
watakuambia uchukue pikipiki
hadi msikiti wa kichangani, hapo
utapelekwa kwenye nyumba
moja fulani hivi amabayo ni
nzuri kidogo kulinganisha na
nyumba za jirani,
nasikia ukiingia tu humu ndani
lazima ulizwe, nasikia
wameweka dawa hapo
mlangoni, na hii nyumba
wanaitumia kama ofis yao ya
kuwatapeli watu hawaish hapo
wala kulala hapo, kwahiyo
kuwapata ni ngumu sana,
Hii ndio nyumba ambayo
ukiingizwa tu lazima ulizwe, ipo
mtongani kichangani ndani
ndani

No comments:

Post a Comment